Kamati ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa inayochunguza utekelezwaji wa
vikwazo vya Baraza la Usalama la umoja huo katika nchi za Somalia na
Eritrea imedai kwamba Asmara imekuwa ikutumia wababe wa kivita ili
kuhujumu amani nchini Somalia. Kamati hiyo imetaja baadhi ya wababe wa
kivita wa Somalia ambao hupokea fedha na taarifa za kiintelijensia
kutoka Eritrea na kusema kuwa, fedha na taarifa hizo hutumiwa na makundi
yenye misimamo mikali kutekeleza mashambulizi nchini Somalia.
Wataalamu
wa UN pia wamesisitiza kwamba Eritrea bado ina uhusiano wa moja kwa
moja na kundi la kigaidi la al-Shabab. Eritrea kwa upande wake
imekanusha madai hayo na kusema yanachochewa kisiasa na nchi jirani ya
Ethiopia. Asmara imesisitiza kuwa haina uhusiano wowote na makundi ya
kigaidi kokote duniani na kwamba vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi yake
si halali na imetaka vikwazo hivyo kuondolewa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment