Rais Abdelaziz Bouteflika wa Algeria, ametoa msamaha kwa maelfu ya
wafungwa kwa mnasaba wa kuwadia sherehe za kumbukumbu za uhuru wa nchi
hiyo. Rais Bouteflika ambaye bado anaendelea kupata matibabu nchini
Ufaransa, alitoa msamaha huo hapo jana kwa mnasaba wa kumbukumbu za
miaka 51 ya uhuru wa taifa hilo. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wafungwa
waliopata msamaha ni 5, 600 ambao walikuwa ima tayari wamekwishatumikia
kifungo au ndio kwanza walikuwa wamehukumiwa.
Hata hivyo wafungwa ambao
wanahusika katika uvunjifu wa amani na maridhiano ya kitaifa nchini au
kuhusika katika jinai maalumu ikiwemo vitendo vya kigaidi,
hawatoachiliwa huru. Zimepita siku 70 huku Rais Abdelaziz Bouteflika
akiendelea kusalia Ufaransa kwa matibabu ya mshituko wa ubongo. Hivi
karibuni vyama na makundi ya kisiasa yanayopinga serikali ya Algeria
vilitaka kufanyika uchaguzi wa kabla ya wakati kwa mujibu wa katiba
kutokana na kuugua rais huyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment