Katibu Mkuu wa Chama tawala nchini Afrika Kusini ANC Bw. Gwede Mantashe, amesema serikali ya Pretoria imeamua kuwekeza zaidi katika nchi za China na India na amesisitiza kuwa Afrika Kusini haina haja na fedha za Wamagharibi. Mantashe ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa nchi nyingi barani Afrika zimegeuza dira zao za kibiashara na kuzielekeza Mashariki kutokana na ubabe wa Wamagharibi katika medani ya biashara. Katibu Mkuu wa ANC ameashiria misimamo ya kindumakuwili ya Marekani na nchi za Ulaya zilizolikoloni bara la Afrika na kusema kuwa bara hilo sasa limezinduka. Amekosoa masharti magumu yanayowekwa na nchi za Magharibi katika miamala ya kibiashara na nchi za Afrika na kuzitaka nchi za bara hilo kuwageukia Wachina kwa ajili ya mahitaji yao ya kibiashara.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment