Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Monday, July 16, 2012

Maandamano yaendelea katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu

Maandamano katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni yamezidi kuingia kasi, kulalamikia ukosefu wa uadilifu na hali mbaya ya kiuchumi.
Televisheni ya Russia Today imeripoti kuwa, maandamano ya maelfu ya wakazi wa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni yameendelea katika maeneo tofauti kulalamikia ughali wa maisha, ukosefu wa uadilifu na kushinikiza kufanyika marekebisho ya kimsingi ya uchumi wa Israel.
Maandamano hayo yameendelea huku raia mmoja wa utawala wa Kizayuni akiwa amejichoma moto kwenye maandamano yaliyofanyika mjini Tel Aviv.
Moshe Silman (57) alijimwagia mafuta ya taa na kujichoma moto siku ya Jumamosi.
Hivi sasa yuko katika hali mbaya kwenye hospitali ya Sheba, baada ya mwili wake kuungua kwa asilimia 90.
Kabla ya kujichoma moto, Mzayuni huyo aliandika barua akisema kuwa viongozi wa Israel wanawaibia maskini na kuwatajirisha zaidi matajiri.

No comments: