Siku kadhaa zilizopita kulienea habari za kuendelea mapigano kati ya magaidi wa Syria na wanajeshi tiifu kwa serikali ya nchi hiyo, yaliyojiri katika maeneo tofauti ya nchi hiyo na kupelekea watu kadhaa kuuawa na wengine wengi kujeruhiwa. Katika hali hiyo Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Syria ametangaza habari ya kuongezeka vitendo vya kigaidi vinavyolenga kukwamisha makubaliano ya usitishwaji mapigano nchini humo. Jihad Maqdisi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo amesema kuwa, tangu ulipotiwa saini mpango wa Kofi Annan, Mjumbe wa Pamoja wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu katika mgogoro wa Syria, mnamo tarehe 12 Aprili 2012 magaidi tayari wamevunja makubaliano hayo mara 3500.
Matukio ya Syria yanaonyesha kuwa, makundi ya kigaidi yanatumia vibaya makubaliano ya usitishaji mapigano kwa ajili ya kupanua zaidi wigo wa vitendo vyao vya uharibifu na ugaidi na yamekusudia kueneza ugaidi huo katika miji ya Damascus na Halab ambayo ni vitivo muhimu vya kisiasa na kiuchumi nchini Syria. Kuendelea kwa vitendo vya kigaidi na mauaji ya jumla dhidi ya raia wasio na hatia na kuwaua kwa kuwavizia shakhsia wa kidini nchini humo, akiwemo Sheikh Abbas Laham aliyekuwa imam wa jamaa katika Haram ya Ruqaiyyah (as) aliyeuawa mwanzoni mwa wiki iliyopita mjini Damascus, kwa mara nyingine kumeonyesha kuwa, magaidi hao hawasiti kutenda jinai yoyote katika kufikia malengo yao. Mambo yaliyotajwa ni katika mfululizo wa njama hatari ambazo zimewalenga moja kwa moja wananchi na kadhalika usalama wa Syria. Inaonekana wazi kuwa, magaidi wa Syria wanapinga mpango wa Kofi Annan Mjumbe wa Pamoja wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu katika mgogoro wa nchi hiyo, unaozitaka pande zote kukomesha machafuko ili kuanza duru ya mazungumzo ya kisiasa. Kwa ajili hiyo magaidi hao kwa kupata uungaji mkono kutoka kwa baadhi ya madola ya Magharibi na nchi zinazofuata siasa za madola hayo zikiwemo Uturuki, Qatar na Saudi Arabia, wanaendelea na vitendo vya utumiaji mabavu na mauaji kuwalenga wanajeshi na raia wasio na hatia nchini Syria. Itakumbukwa kuwa, kufuatia kutiwa saini mpango wa usitishaji mapigano nchini humo, tarehe 12 mwezi uliopita Kofi Annan alitangaza usitishaji mapigano nchini humo. Hata hivyo, licha ya kuwepo waangalizi wa Kimataifa wapatao 260 nchini humo lakini bado magaidi hao wanazidi kuvunja makubaliano hayo kila uchao. Hii ni katika hali ambayo serikali ya Damascus chini ya uongozi wa Rais Bashar Al Asad imejitahidi kuufanyia kazi mpango wa Kofi Annan kwa minajili ya kumaliza kabisa mgogoro nchini humo. Imekuwa ikishirikiana vyema na waangalizi wa Kimataifa nchini Syria, hali iliyoipelekea tume ya waangalizi wa Umoja wa Mataifa kuishukuru serikali hiyo kuhusu suala hilo. Waangalizi wa Umoja wa Mataifa wanasisitiza kuwa, shughuli zao nchini Syria zinaweza kurejesha hali ya amani nchini humo, na kwamba jambo hilo linahitajia kwanza ushirikiano kamili kutoka kwa pande zinazolumbana katika mgogoro wa nchi hiyo. Kwa ajili hiyo ushirikiano wa serikali ya Damascus na tume ya waangalizi hao wa Umoja wa Mataifa pekee hautoshi, bali magaidi wanaoendelea kutoa roho za watu bila huruma nchini humo pia wanapaswa kulazimishwa kusimamisha mara mora mauaji ya kinyama dhidi ya watu wasio na hatia na kuketi kwenye meza ya mazungumzo na serikali halali ya Damascus ili kurejesha amani na uthabiti wa kisiasa nchini humo.

No comments:
Post a Comment