Serikali ya Sudan imetangaza kuwa, haitotekeleza vitisho ilivyokuwa
imevitoa hapo kabla dhidi ya Sudan Kusini, juu ya kufunga mabomba ya
usafirishaji mafuta ya nchi hiyo katika ardhi yake. Hayo yamesemwa na
Rabiu Abdul-Aatwi mmoja wa viongozi wa Chama cha Kongresi ya Kitaifa cha
Sudan na kuongeza kuwa, hatua hiyo imekuja baada ya makubaliano
yaliyofikiwa katika kikao cha wiki iliyopita kati ya Makamu wa Rais wa
Sudan Kusini Riek Machar na Ali Othman Taha, Makamu wa Rais wa Sudan.
Mwanzoni mwa mwezi Juni mwaka huu, serikali ya Khartoum ilitishia
kusimamisha usafirishaji wa mafuta ya Sudan Kusini na kutoa fursa ya
siku 60 kabla ya kuanza hatua hiyo. Hatua hiyo ilichukuliwa baada ya
Rais Omar Hassan Ahmad Al-Bashir wa Sudan kuituhumu Sudan Kusini kwa
kuwaunga mkono waasi dhidi ya nchi yake. Hata hivyo serikali ya Juba
ilipinga vikali tuhuma hizo na kuzitaja kuwa, zisizo na ukweli wowote
ule.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment