![]() |
Mkuu wa Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa |
Mkuu wa Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, Navi Pillay ameitaka serikali ya Zimbabwe ichukue hatua za kuzuia kujikariri machafuko ya kisiasa yaliyoshuhudiwa mwaka 2008. Pillay ameyasema hayo baada ya mazungumzo yake na Waziri Mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai mjini Harare. Navi Pillay amesema Zimbabwe haina budi kuhakikisha kwamba uchaguzi mkuu ujao utakuwa huru na wa haki ili kuepuka kutokea machafuko ya kisiasa. Amesema serikali ya Harare imepiga hatua katika suala la haki za binadamu ingawa amesisitiza kuwa bado kuna kibarua cha ziada kinachowakodolea macho viongozi wa serikali ya muungano nchini humo. Pillay anaongoza ujumbe wa ngazi za juu wa Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa ambao unafanya ziara ya siku tano nchini Zimbabwe.
No comments:
Post a Comment