Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Monday, July 16, 2012

Hali bado ni tata Mali, Algeria yaimarisha ulinzi kwenye mpaka wake na Mali

Hali bado ni tata nchini Mali licha ya waasi wa kaskazini mwa nchi hiyo kulegeza misimamo yao na kusema kuwa hawana tena nia ya kutaka kujitenga na nchi hiyo. Serikali ya Algeria yenye mpaka mkubwa na Mali imeimarisha ulinzi kwa kupeleka zana nzito za kijeshi kwenye mpaka wake na nchi hiyo na kutangaza kuwa iko tayari kukabiliana na hali yoyote isiyo ya kawaida. Kwa upande wake, Rais Francois Hollande wa Ufaransa amesema kuwa, ni juu ya Waafrika wenyewe kuamua ni vipi na ni wakati gani inabidi kuingilia kijeshi huko Mali kwa ajili ya kupambana na waasi wa kaskazini mwa nchi hiyo. Matamshi hayo ya Hollande yanadhihirisha wazi jinsi mkoloni mkongwe wa Ulaya yaani Ufaransa anavyojipa haki ya kuingilia masuala ya nchi za Afrika kama alivyofanya nchini Ivory Coast na ni ishara ya wazi ya kuwa yuko tayari kutuma wanajeshi wake kaskazini mwa Mali. Hali hiyo imejitokeza huku kukiwa na taarifa kuwa wanadiplomasia watatu kati ya 7 wa Algeria waliotekwa nyara na waasi wa Mali mwezi Aprili mwaka huu, wameachiliwa huru. Wakati huo huo viongozi wa nchi za Afrika wamewataka wanajeshi waliofanya mapinduzi nchini Mali kuunda serikali ya mpito itakayoweza kukabiliana na waasi wa kaskazini mwa nchi hiyo.

No comments: