Spika wa Bunge la Syria amesema kuwa, Jumuiya ya Nchi za Kiarabu ni
chombo kinachotumiwa na viongozi wa Ghuba ya Uajemi kwa ajili ya kufikia
malengo yao. Mohammad Jihad al-Laham ameongeza kuwa, Jumuiya ya Nchi za
Kiarabu inayojulikana kwa jina la Arab League ni wenzo wa viongozi wa
Ghuba ya Uajemi wenye fikra finyu kwa ajili ya kufikia malengo yao ya
kisiasa. Spika wa Bunge la Syria ametahadharisha kuhusiana na njama za
kugawanywa nchi za Mashariki ya Kati na kusema kwamba, nchi za eneo la
Mashariki ya Kati zinakabiliwa na hatari ya kugawanya.
Spika huyo wa
Bunge la Syria amezikosoa vikali siasa za viongozi wa Ghuba ya Uajemi na
njama zao za kuitumia Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kama wenzo wao wa
kufikia malengo ya kisiasa. Amesema, Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imesahau
hata kadhia muhimu ya Palestina na dhulma wanayotendewa wananchi
madhlumu wa Palestina na utawala wa Kizayuni wa Israel. Amesema,
inasikitisha kuona nchi hizo zinawaunga mkono magaidi wanaoendesha
harakati zao nchini Syria na kupiga ngoma ya kutumiwa nguvu za kijeshi
dhidi ya Syria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment