Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Wednesday, May 23, 2012

AMISOM yasema imechukua udhibiti wa mji wa Afgooye nchini Somalia

Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM kimedai kuchukua udhibiti wa mji muhimu wa Afgooye ulioko magharibi mwa mji mkuu Mogadishu. Taarifa ya AMISOM imesema kuwa walinda amani wa Umoja wa Afrika (AU) wamedhibiti mji huo baada ya mapigano makali na kundi la Ash-shabab. Taarifa hiyo pia imesema oparesheni ya kuukomboa mji wa Afgooye imefanywa kwa ushirikiano na jeshi la serikali ya Somalia. Hakuna habari zilizotolewa kuhusiana na waliouawa au kujeruhiwa kwa upande wa AMISOM au Ash-shabab. Kundi la Ash-shabab lenye mfungamano na mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda linapigania kuipindua serikali ya mpito ya Somalia kwa madai kuwa serikali hiyo ni kibaraka wa nchi za Magharibi hususan Marekani.

No comments: