Rais Adly Manosur wa serikali ya mpito ya Misri ameapisha serikali ya
kwanza ya nchi hiyo tangu jeshi limpindue rais wa zamani wa nchi hiyo
Mohamed Morsi wiki mbili zilizopita. Hazem el Beblawi, mchumi mwenye
fikra za kiliberali jana jioni alikula kiapo mbele ya Rais Adly Mansour
kuongoza serikali ya mpito ya Misri akiwa Waziri Mkuu Mpya.
Aidha Abdul
Fatah as Sisi, mkuu wa jeshi la Misri ambaye aliongoza mapinduzi dhidi
ya Morsi amekula kiapo cha kuwa Makamu wa Kwanza wa Waziri Mkuu huku
akiendelea kushikilia wadhifa wake wa Waziri wa Ulinzi. Naye Nabil Fahmy
ambaye alikuwa balozi wa Misri mjini Washington kuanzia mwaka 1999 hadi
2008 ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje huku Mohammed Ibrahim
aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa serikali ya Morsi akisalia katika
wadhifa huo. Baraza jipya la mawaziri la serikali ya mpito ya Misri
limewajumuisha pia wanawake watatu akiwemo Waziri wa Afya Maha ar Rabat.
Wakati huo huo harakati ya Ikhwanul Muslimin ya Misri imepinga baraza
hilo jipya la mawaziri ikisema kuwa serikali hiyo si halali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment