Serikali mpya ya Misri imeitaka Uturuki kukoma mara moja kuingilia mambo
yake ya ndani. Hii ni baada ya Waziri Mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip
Erdogan kusema mara kadhaa kwamba nchi yake bado inamtambua Mohammad
Mursi kuwa rais halali wa Misri. Jumapili iliyopita, Erdogan aliiambia
kanali moja ya televisheni ya Uturuki kwamba Ankara haiwezi kuunga mkono
mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika Misri majuma mawili yaliyopita.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri imetoa taarifa na kuyataja matamshi hayo
ya Erdogan kuwa uingiliaji wa mambo ya ndani ya nchi hiyo na kumtaka
kiongozi huyo kuacha kabisa tabia hiyo. Dkt. Muhammad Mursi alikuwa
muitifaki mkubwa wa Waziri Mkuu wa Uturuki hususan katika kadhia ya
Syria na kuondolewa kwake madarakani kumetoa pigo kubwa kwa kiongozi
huyo na serikali ya Ankara kwa ujumla.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment