Waziri wa Fedha wa Sudan ameuomba Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF)
kuisaidia nchi yake. Abdurrahman Sarar, Waziri wa Fedha wa Sudan
amesema, chanzo kikuu cha matatizo ya hivi sasa ya kiuchumi wa Sudan ni
vikwazo na madeni ya kigeni kwa nchi hiyo. Abdurrahman Sarar ameiomba
IMF kuisaidia Sudan kuinua uchumi wake.
Waziri wa Fedha wa Sudan
amesema, uchumi wa nchi hiyo kwa asilimia mia moja unategemea mapato ya
kigeni. Abdurrahman Sarar ameashiria pia safari za ujumbe wa IMF huko
Khartoum na kueleza kuwa, pande mbili za IMF na Sudan zimefikia
makubaliano mbalimbali ili kuweza kutataua matatizo ya kiuchumi ya
Sudan. Waziri huyo wa Fedha wa Sudan amesema, uchumi wa nchi hiyo
umeboreka kwa kiwango fulani mwaka huu ikilinganishwa na mwaka uliopita.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment