Leo ni Akhamisi tarehe 9 Ramadhani 1434 Hijria, sawa na Julai 18, 2013.
Siku kama ya leo miaka 25 iliyopita Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
ilikubali azimio nambari 598 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Azimio hilo lilizitaka nchi mbili za Iran na Iraq kusitisha vita na
kufanya suluhu. Jamhuri ya Kiislamu ilikubali azimio hilo kutokana na
baadhi ya vipengele vyake hususan kile kinachohusiana na kuitambulisha
Iraq kuwa ndiye
mchokozi katika vita hivyo na kuitaka iilipe Iran fidia
za hasara za vita hivyo. Hata hivyo utawala wa Saddam Hussein ambao pia
ulikubali azimio hilo la Baraza la Usalama, uliendeleza mashambulizi
dhidi ya ardhi ya Iran.
Tarehe 18 Julai miaka 230 iliyopita William Herschel, mtaalamu
maarufu wa nujumu wa Uingereza alifanikiwa kugundua hakika ya kundi la
nyota na sayari ikiwemo hii yetu ya dunia la Galaxy. Alitumia darubini
kubwa aliyokuwa ametengeneza kwa ajili ya kutazama nyota na kuthibitisha
kwamba, kundi la nyota na sayari la Galaxy linaundwa na nyota nyingi
ikiwemo sayari ya dunia ambao ni sehemu ndogo sana ya kundi hilo.
Aligundua kwamba, kundi hilo la nyota na sayari zinatembea na kuzunguka
kwa pamoja angani. Herschel pia ndiye mvumbuzi wa sayari ya Uranus.
Alifariki dunia mwaka 1822 akiwa na umri wa miaka 84.
Na siku kama ya leo miaka 1142 iliyopita kilianza kipindi cha vita
vya miaka 25 kati ya Uingereza na Denmark katika karne ya 9. Alfred The
Great, mfalme kijana wa Uingereza alikuwa kamanda mashuhuri wakati wa
kujiri vita hivyo katika kipindi hicho. Wadenmark katika siku hiyo
waliivamia Uingereza na kuiteka ardhi kubwa ya nchi hiyo. Vita hivyo
vilivyodumu kwa miaka 25 hatimaye vilitia ukomo kwa Waingereza kupata
ushindi mnamo tarehe 9 Januari mwaka 896.
No comments:
Post a Comment