Umoja wa Afrika (AU) umetoa wito wa kuzidishwa juhudi za kung'oa mizizi ya ugaidi nchini Somalia.
Mjumbe malumu wa Umoja wa Afrika katika masuala ya Somalia Mahamat
Saleh Annadif amesisitiza kuwa nchi za Kiafika zinapaswa kushirikiana
zaidi katika kupambana na ugaidi nchini Somalia.
Amesema ugaidi haujui mipaka ya nchi na ametoa wito wa kuwepo ushirikiano na mikakati mikubwa zaidi ya kupambana nao.
Wapiganaji wa kundi la al Shabaab wanaodhibiti baadhi ya maeneo ya
Somalia wamekuwa wakijitangaza kuwa na uhusiano la kundi la kigaidi la
al Qaida. Wapiganaji wa kundi hilo wamekuwa wakishambulia maeneo
mbalimbali ya Somalia na hata katika nchi jirani na kuua watu wasio na
hatia kwa kutumia visingizio mbalimbali.
No comments:
Post a Comment