Rais Mahmoumd Ahmadinejad wa Iran amesema kuwa watu wote wanapaswa kuheshimu kura na matashi ya wananchi.
Rais Ahmadinejad ambaye alikuwa akihutubia hadhara ya mabalozi na
wawakilishi wa nchi za Kiislamu mjini Tehran ameashiria hali ya mambo
katika baadhi ya nchi za Waislamu na akesema, njia pekee ya kupatikana
haki za kimsingi ni maelewano na udugu.
Amesema uadilifu, uhuru na
utukufu haviwezi kupatikana kwa njia ya mauaji, mapigano na vita
vinavyoua watu na kuharibu uchumi, mbali na kupandikiza vinyongo katika
roho za watu. Amesema viongozi wanaotwaa madaraka kwa njia ya vita
wanajipalilia njia ya kuondolewa madarakani kwa njia hiyo hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu mesema, Waislamu wana maadui wa
kihistoria na kwamba Wazayuni ndio maadui wa mataifa yote ya Kiislamu.
Amesisitiza kuwa Wazayuni hawayatakii mema mataifa yote ya Kiislamu.
Vilevile amewahimzia Waislamu kufaidika na baraka za mwezi huu
mtukufu wa Ramadhani na kusema, kufanya ibada katika mwezi huu ambamo
shetani amefungwa minyororo na milango ya rehma za Mwenyezi Mungu
imefunguliwa, ni bora mara kadhaa kuliko kufanya ibada katika miezi
mingine ya mwaka.
No comments:
Post a Comment