Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya Catherine Ashton ameutaka
utawala wa sasa wa Misri kumuachia huru rais aliyeondolewa madarakani wa
nchi hiyo Muhammad Mursi na wanasiasa wengine wanaoshikiliwa na jeshi
la nchi hiyo.
Ashton alitoa wito huo jana mjini Cairo katika mazungumzo yake na
viongozi wapya wa Misri akiwemo Rais wa muda wa nchi hiyo Adly Mansour.
Catherine Ashton amewaambia waandishi habari kwamba, amewataka
viongozi wa sasa wa Cairo kumwachia huru Mursi na wanasiasa wengine wa
Harakati ya Ikhwanul Muslimin kama hawakabiliwi na tuhuma za aina
yoyote. Amesema alitaka kukutana na Mursi anayeshikiliwa na jeshi mahala
pasipojulikana, lakini hakufanikiwa.
Wakati huo huo maelfu ya wananchi wa Misri wameendelea kufanya
maandamano katika miji mbalimbali ya nchi hiyo wakitaka kurejeshwa
madarakani Muhammad Mursi.
No comments:
Post a Comment