Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Friday, July 19, 2013

Al-Sisi aliitaarifu Israel kabla ya kumpindua Mursi

Rooney Daniel mchambuzi wa masuala ya kijeshi wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel, amefichua kuwa, Abdul Fatah as Sisi, Waziri wa Ulinzi wa Misri, aliitaarifa Israel kuwepo njama za kumpindua Rais Muhammad Morsi wa nchi hiyo siku tatu kabla ya tukio hilo. Akizungumza kupitia kanali ya pili ya televisheni ya utawala huo, Rooney Daniel amesema kuwa,
as Sisi aliutaka utawala wa Kizayuni kuimarisha ulinzi dhidi ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS kwa kukhofia kuwa, inaweza kutoa radiamali kali dhidi ya Misri. Aidha amesema kuwa, as Sisi aliwambia viongozi wa Tel Aviv kwamba, anaiogopa harakati ya Hamas na Israel ilimuhakikishia waziri huyo wa ulinzi wa Misri kwamba, itaweka ulinzi mkali katika mipaka ya Ukanda wa Ghaza ili kuzuia hatua zozote zinazoweza kuchukuliwa na HAMAS. Kwa upande wake utawala wa Kizayuni wa Israel ulimtaka as Sisi kuharibu njia za chini kwa chini zinazotumiwa na wakazi wa Ukanda wa Ghazas mkabala na ulinzi huo wa Israel. Daniel amefafanua zaidi kuwa, mapinduzi ya kijeshi dhidi ya Mursi, ni kwa maslahi ya utawala wa Kizayuni wa Israel na ni katika kuudhaminia usalama utawala huon ghasibu.

No comments: