Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan amesisitiza
ulazima wa kufanyiwa marekebisho muundo wa Baraza la Usalama la Umoja wa
Mataifa.
Annan amesisitiza kuwa, muundo wa hivi sasa wa Baraza la Usalama ni
wa zamani, kwani unakidhi mahitaji yaliyokuweko katika muongo wa 90,
hivyo unapaswa kubadilishwa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu
chake huko Moscow nchini Russia, katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa
Mataifa amesema kuwa, India pamoja na kuwa na zaidi ya watu bilioni
moja, haina kiti kwenye baraza hilo. Ameongeza kuwa, inashangaza kuona
pia nchi za Kiafrika na zile za Amerika ya Latini nazo hazina kiti cha
kudumu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Kuhusu mgogoro wa Syria, Kofi Annan ambaye aliwahi kuwa mjumbe wa
Umoja wa Mataifa kwenye mgogoro wa nchi hiyo amesema kuwa, nchi zote
wanachama wa Umoja wa Mataifa zinapaswa kuwa na sauti moja katika kuunga
mkono mpango wa kufanyika mkutano wa kimataifa wa Geneva 2 wenye lengo
la kuukwamua mgogoro wa Syria.
No comments:
Post a Comment