Mapigano makali yaliyojiri kati ya majeshi ya serikali ya Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo na waasi wa kundi la M23 katika kipindi cha
masaa 48 yaliyopita, yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 130 karibu
na mji wa Goma, ulioko katika jimbo la Kivu Kaskazini.
Hayo yamesemwa na Lambert Mende Omalanga Waziri wa Habari na msemaji
wa serikali ya Kongo wakati alipozungumza na waandishi wa habari mjini
Kinshasa.
Omalanga ameongeza kuwa, mapigano makali yalishuhudiwa katika
eneo la Mutaho lililoko umbali wa kilomita 7 kaskazini mwa Goma kati ya
vikosi vya jeshi la serikali na waasi na M23, na kwamba hatimaye vikosi
vya serikali ya Kinshasa vimefanikiwa kuwaangamiza waasi 120, kuwatia
mbaroni waasi 12 na makumi ya wengine kujeruhiwa.
Omalanga ameongeza kuwa, wanajeshi 10 wa serikali pia waliuawa.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, mwezi Novemba mwaka jana, kundi la waasi wa
M23 lilifanikiwa kuuteka mji wa Goma na kuukalia kwa mbavu kwa muda wa
siku 10, lakini lililazimika kuondoka baada ya kukabiliwa na
mashinikizo makubwa ya nchi za eneo la Ukanda wa Maziwa Makuu ya Afrika.
No comments:
Post a Comment