Kwa akali watu 22 wameuawa nchini Afghanistan na makumi ya wengine
kujeruhiwa kufuatia mashambulio mawili tofauti ya anga yaliyofanywa na
majeshi ya NATO nchini humo. Taarifa zaidi zinasema kuwa, vikosi vya
Jumuiya ya Kijeshi ya NATO vimefanya mashambulio makubwa katika majimbo
ya Paktia na Ghazni na kusababisha mauaji hayo.
Msemaji wa Gavana wa
jimbo la Ghazni Nabil Jan amesema kuwa, raia 10 wameuawa katika
shambulio lililofanywa na vikosi vya NATO katika kijiji cha Khogian.
Wakati huo huo, Kamanda wa polisi wa jimbo la Paktia naye amethibitisha
majeshi ya NATO kufanya mashambulio katika jimbo hilo na kuongeza kuwa,
watu wasiopungua 12 wameuliwa katika shambulio hilo. Ameongeza kuwa, mji
uliolengwa na mashambulio hayo ya NATO katika jimbo la Paktia ni wa
Zarmat.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment