Kikosi cha kusimamia amani cha Umoja wa Mataifa kilichoko katika Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Congo kimetangaza kuwa, kimejiandaa kikamilifu
kupambana na waasi wa M23 ili kuwazuia wasisonge mbele kuelekea katika
mji wa Goma. Kikosi hicho maalumu cha askari 3000 kutoka Tanzania,
Malawi na Afrika Kusini kina jukumu la kulinda roho za raia mkabala na
mashambulio ya waasi wa M23.
Kikosi hicho ambacho kimeruhusiwa
kuwashambulia waasi hao wa M23 kimesema kuwa, kimejiandaa kikamilifu
kukabiliana na hatua yoyote ya waasi hao ya kutaka kusonga mbele
kuelekea mjini Goma. Wakati huo huo, mapigano makali yaliyojiri kati ya
majeshi ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na waasi wa M23
katika kipindi cha masaa 48 yaliyopita, yamesababisha vifo vya watu
wasiopungua 130 karibu na mji wa Goma, ulioko katika jimbo la Kivu
Kaskazini. Hayo yamesemwa na Lambert Mende Omalanga Waziri wa Habari na
msemaji wa serikali ya Congo wakati alipozungumza na waandishi wa
habari mjini Kinshasa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment