Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini Tanzania, Jaji Joseph
Warioba amesema iwapo Mfumo wa Serikali Tatu utaridhiwa na wananchi ni
lazima mambo yaliyo ndani ya Muungano yatagawanywa ikiwa ni pamoja na
Ikulu ya Rais. Amesema kutokana na taifa kufanya mabadiliko ya Katiba ni
lazima kuwepo mpangilio wa kugawana mambo mbalimbali yaliyokuwa chini
ya Muungano ikiwamo majengo, wafanyakazi, Ikulu, hata vitendea kazi na
kwamba utaratibu huo ni kama ule uliotumika wakati Tanganyika na
Zanzibar zilipoungana. Kauli ya hiyo ya Jaji Warioba imekuja siku tatu
tangu Waziri wa Katiba na Sheria,
Mathias Chikawe kueleza kuwa Tanzania
Bara itaanza mchakato wa kutunga Katiba yake Aprili mwaka 2014 na
kumalizika Desemba mwaka huohuo. Jaji Warioba aliyasema hayo katika
mahojiano maalumu na waandishi wandamizi wa habari jijini Dar es salamu,
Tanzania. Hata hivyo aliongeza kuwa suala hilo linahitajia mazungumzo
ya pande zote mbili, baada ya kukamilika kwa mchakato huu kwa sababu hii
ni rasimu tu, ambayo itajadiliwa na wananchi kabla ya kuanza kwa Bunge
la Katiba na baadaye kuwepo kwa kura ya maoni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment