Leo ni Jumamosi tarehe 28 Rajab mwaka 1434 Hijiria, inayosadifiana na tarehe 8 Juni 2013 Miladia.
Siku kama ya leo miaka 118 iliyopita alizaliwa mwandishi na mhakiki
mkubwa wa Kiirani Said Nafisi katika mji wa Tehran. Baada ya kupata
elimu ya upili, Nafisi alielekea Ufaransa kwa ajili ya elimu ya juu.
Alirejea nchini baada ya kukamilisha masomo na kufundisha katika vyuo
vikuu hapa nchini. Said Nafisi ameandika na kutarjumu vitabu zaidi ya
180 ikiwemo kamusi ya Kifaransa na Kifarsi.
Siku kama ya leo miaka 158 iliyopita, sehemu kubwa ya mji mkuu wa
Ureno Lisbon iliharibika kutokana na mtetemeko mkubwa wa ardhi na moto
uliosababishwa na zilzala hiyo. Karibu wakazi elfu arubaini wa mji huo
walipoteza maisha yao na theluthi mbili ya nyumba na taasisi za kiuchumi
za mji huo kubomoka. Mbali na maafa hayo, karibu meli elfu mbili, boti
na ngalawa nyingi zilizokuwa katika bandari za Ureno zilighiriki.
Mtetemeko huo ni moja ya mitetemeko mikubwa zaidi kuwahi kuikumba Ureno.
Na miaka 21 iliyopita muwafaka na leo, shirika la ujasusi la Israel Mossad lilitekeleza mauaji mengine ya kigaidi dhidi ya viongozi wa Palestina katika mojawapo ya nchi za kigeni. Siku hiyo maajenti wa Mossad walimuuwa Atef Bseiso ambaye alikuwa miongoni mwa maafisa usalama wa PLO huko Paris, Ufaransa. Licha ya kutokuwepo shaka juu ya kuhusika Israel katika mauaji hayo, lakini utawala huo ghasibu ulikana kufanya jinai hiyo ya kinyama kwa kuchelea hasira za walimwengu. Hata hivyo miaka saba baadaye, polisi ya Ufaransa ilitangaza kwamba shirika la ujasusi la Israel Mossad ndilo lililopanga na kutekeleza mauaji hayo.

No comments:
Post a Comment