Maelfu ya wapinzani na waungaji mkono wa Rais Muhammad Morsi
wamefanya maandamano mjini Cairo, Misri. Taarifa zinasema kuwa,
wanaharakati wa kisiasa wa makundi ya Kisalafi na baadhi ya makundi
yenye misimamo ya Kiislamu inayokaribiana na harakati ya Ikhwanul
Muslimiin yamefanya maandamano ya kuunga mkono maamuzi yaliyochukuliwa
hivi karibuni na Rais Morsi wa nchi hiyo. Waandamanaji hao walikusanyika
mkabala wa Masjidul Rabi'i al A'dawiya mjini Cairo, na kutaka
itekelezwe sheria za Kiislamu nchini humo.
Kwa upande mwingine, wapinzani wa Rais Morsi walikusanyika mkabala wa
Wizara ya Ulinzi wakilalamikia maamuzi yaliyochukuliwa hivi karibuni na
kiongozi wa nchi hiyo. Duru mpya ya maandamano nchini Misri
imeshuhudiwa baada ya Rais Morsi kufanya mabadiliko ya Magavana wa
majimbo kadhaa nchini humo. Wapinzani wanadai kwamba shakhsia wengi wa
Kisalafi na Ikhwanul Muslimin wamepewa nyadhifa muhimu nchini humo.
No comments:
Post a Comment