Khatibu wa sala ya Ijumaa hapa mjini Tehran amesema kuwa duru ya 11 ya
uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni ushindi adhimu kwa
taifa la Iran katika chimbuko la hamasa ya kisiasa. Ayatullah Muhammad
Ali Muvahidi Kermani Khatibu wa sala ya Ijumaa ya mjini Tehran amesifu
na kuwashukuru wananchi wa Iran ya Kiislamu kwa kushiriki kwa wingi
katika hamasa ya kisiasa na kueleza kuwa hamasa hiyo ilikuwa itikio kwa
wito wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa ajili ya
kushiriki katika uchaguzi huo wa rais.
Ayatullah Muvahidi Kermani
amesisitiza kuwa hamasa ya kisiasa ya Juni 14 2013 kwa mara nyingine
tena imelipa heshima na fakhari taifa la Iran na kupelekea kushindwa
maadui wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Khatibu wa sala ya Ijumaa ya Tehran pia amempongeza Sheikh Dakta
Hassan Ruhani Rais mteule wa Iran na kumtaja kuwa kiongozi shupavu,
mfuasi wa utawala wa faqihi na mwenye rekodi nzuri kabla na baada ya
ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
No comments:
Post a Comment