Makundi ya kisiasa nchini Afrika Kusini yameitaja Marekani kuwa mporaji
wa maliasili na utajiri wa nchi za Kiafrika, na yamepinga safari
inayotarajiwa kufanywa na Rais Barack Obama wa Marekani nchini humo siku
chache zijazo. Muungano wa wafanya biashara nchini Afrika Kusini COSATU
umewataka wafanyakazi nchini humo kufanya maandamano ya kupinga safari
hiyo. Bongani Masuku katibu wa masuala ya kimataifa wa COSATU amesema
kuwa, siasa za Marekani zimejikita zaidi katika kuzalisha na
kukithirisha silaha za nyuklia na kusambaza silaha ulimwenguni, jambo
ambalo linavuruga amani, uadilifu, demokrasia na haki za binadamu.
Amesema kuwa, Marekani ina majeshi ya kutekeleza oparesheni maalumu
katika nchi kadhaa ulimwengu, hatua ambayo imesababisha ghasia na
machafuko kwenye nchi kadhaa ulimwenguni. Hivi karibuni, Muungano wa
Mawakili wa Kiislamu nchini humo ulivitaka vyombo vya sheria nchini humo
kumtia mbaroni Rais Obama atakapoingia nchini humo kwa tuhuma za
kutenda jinai na ukiukaji wa haki za binadamu katika nchi mbalimbali
duniani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment