Chama kikuu cha upinzani Ethiopia kimetoa wito kwa serikali ya
nchi hiyo kufuta sheria dhidi ya ugaidi ambayo imekuwa ikitumiwa
kuwakandamiza wapinzani. Msemaji wa Chama cha Unity for Democracy and
Justice Daniel Tefera amesema iwapo sheria hiyo haitabatilishwa
wataitisha maandamano makubwa kama yale yaliyoshuhudiwa mjini Addis
Ababa mapema mwezi huu.
Sheria dhidi ya ugaidi iliyopitishwa nchini humo mwaka 2009
inaonekana kuwasakama zaidi wapinzani wa serikali kwa sababu kila
atakayeshapisha taarifa ambazo zinaonekana kuchochea ghasia anaweza
kuhukumiwa kifungo cha baina ya miaka 10 hadi 20 jela. Hadi sasa
waandishi habari 10 wamefikishwa mahakamani kwa msingi wa sheria hiyo
dhidi ya ugaidi.
Serikali ya Ethiopia inasema sheria hiyo ni muhimu katika kukabiliana
na waasi wanaotaka kujitenga ambao wanaoungwa mkono na nchi jirani ya
Eritrea.
No comments:
Post a Comment