Mamia ya raia wa Ivory Coast wameandamana mjini Abidjan kumuunga mkono
Rais wa zamani wa nchi hiyo, Laurent Gbagbo na kukosoa siasa
zinazofuatwa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC dhidi ya rais wao wa
zamani. Maandamano hayo yalifanyika jana mjini Abidjan, mbele ya
mahakama kuu ya nchi hiyo. Waandamanaji walikuwa wamevaa mashati meupe
ambayo yalikuwa yameandikwa ‘Wahanga wa mgogoro wa uchaguzi’.
Aidha
walibeba mabango yaliyokuwa yameandikwa ujumbe wa kukosoa siasa za
upendeleo zinazofuatwa na Mahakama hiyo ya Jinai ya Kimataifa ya ICC,
katika kuwaandama viongozi wa Afrika pekee. Laurent Gbagbo, Rais wa
zamani wa Ivory Coast anatuhumiwa kutenda jinai dhidi ya binaadamu na
anaendelea kushikiliwa katika korokoro za mahakama hiyo kwa miaka kadhaa
sasa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment