Liberia imetuma wanajeshi karibu 50 huko Mali watakaojiunga na kikosi
cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini humo. Kwa mara ya kwanza
baada ya kumalizika vita vya ndani vya miaka 14, Liberia imetuma
wanajeshi hao wa kulinda amani huko Mali ambao watatekeleza kazi ya
kulinda amani katika fremu ya kikosi cha Umoja wa Mataifa. Wanajeshi wa
kulinda amani wa umoja wa Mataifa zaidi ya elfu 12 wanatazamiwa
kuwasili nchini Mali kuanzia mwezi ujao ili kuchukua nafasi ya vikosi
vya Ufaransa vilivyoko nchini humo.
Kikosi hicho cha walinda amani
kitakuwa na majukumu ya kurejesha amani na uthabiti nchini humo. Rais
Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia amewataka wanajeshi wa nchi hiyo
waliotumwa Mali kuheshimu sheria na kuwa na nidhamu katika muda wote
wakataokuwepo huko Mali katika shughuli za kulinda amani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment