Rais Omar Hasan al Bashir wa Sudan ameonya juu ya hatari ya mapigano ya
kikabila ambayo yamekuwa yakitokea katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo.
Al Bashir ameyasema hayo leo katika kikao cha Baraza la Ushauri la
Kongresi ya Kitaifa na kuongeza kuwa, mapigano hayo ambayo yamekuwa
yakijiri katika baadhi ya maeneo ya nchi yake, ni hatari kubwa kwa
taifa la Sudan na kwamba, serikali yake inakabiliwa na changamoto kubwa
katika kuzuia hali hiyo. Amesema kuwa, baadhi ya watu katika baadhi ya
makabila, wamekuwa wakizusha na kuchochea chokochoko za mapigano hayo ya
kikabila.
Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa, katika miezi ya
hivi karibuni, mapigano ya kikabila na kikaumu katika maeneo tofauti ya
jimbo la Darfur yameshtadi baada ya kupita kupindi kirefu cha utulivu.
Wiki iliyopita watu 40 waliripotiwa kuuawa katika mapigano ya kikabila
jimboni humo. Hii ni katika hali ambayo mwaka 2003, eneo hilo
lilishuhudia mapigano makali yaliyopelekea idadi kubwa ya watu kuuawa na
kujeruhiwa huku maelfu ya wengine wakilazimika kuwa wakimbizi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment