Mamia ya wanaharakati wa kutetea haki za binaadamu mjini Istanbul,
Uturuki, wamefanya maandamao dhidi ya serikali ya nchi hiyo.
Wanaharakati hao walimiminika mabarabarani jana huku wakitoa nara za
kupinga siasa za kidikteta za Recep Tayyip Erdoğan Waziri Mkuu wa nchi
hiyo. Aidha waandamanaji hao walielekea kwenye medani ya Taksim na
kulaana siasa za ukandamizaji zinazotekelezwa na polisi ya nchi hiyo
dhidi ya waandamanaji. Kabla ya hapo pia, maelfu ya wakazi wa mjini
Istanbul walikusanyika katika medani hiyo na kutoa nara za kupinga
serikali inayoongozwa na Erdogan.
Ni vyema kuashiria hapa kuwa, tangu
tarehe 31 Mei nwaka huu, Uturuki imekuwa ikishuhudia wimbi kubwa la
maandamano ya wananchi dhidi ya serikali. Mbali na waandamanaji kupinga
hatua ya kutaka kuharibu bustani ya Gezi, wanalaani vikali pia msimamo
wa Erdogan wa kuunga mkono magaidi wanaotaka kuiangusha serikali ya
wananchi wa Syria. Waturuki sasa wanataka Waziri Mkuu Erdogan ajiuzulu
na kuitishwa uchaguzi wa mapema nchini humo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment