Chama Kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Demokrasia na Maendeleo
Chadema, kimekituhumu chama tawala cha CCM kuwa, kina mpango mchafu wa
kuwabambikizia viongozi wakuu wa chama hicho kesi ya kumwagiwa Tindikali
kada wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Musa Tesha. Chadema kimeongeza kuwa,
Viongozi wanaoandaliwa mpango huo ni pamoja na Mwenyekiti wa chama
hicho, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu, Dakta. Willibrod Slaa, Mbunge wa
Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, Mnyika, wakati
akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, na
kuongeza kuwa, mpango huo unafanyika kwa lengo la kukidhoofisha chama
chao kinachowapa wakati mgumu CCM. Aidha Mnyika amesema, hivi sasa
makachero wa polisi wamekuwa wakiwakamata vijana na kuwalazimisha kukiri
kwa kuandika au kuandikiwa maelezo kuwa viongozi hao waliwatuma
kummwagia tindikali Tesha wakati wa uchaguzi mdogo wa Igunga mwaka 2011.
Alibainisha kuwa, kutokana na kesi hiyo kuonekana kujaa masuala ya
kisiasa, kitashirikiana na mawakili wake kwa ajili ya kukabiliana na
njama hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment