Rais Paul Kagame wa Rwanda amefanya mabadiliko kwenye safu za uongozi wa
jeshi na kumteua Jenerali Patrick Nyamvumba kuwa mkuu mpya wa majeshi
ya nchi hiyo. Jenerali Nyamvumba amechukua nafasi ya Jenerali Charles
Kayonga aliyeshikilia nafasi hiyo tangu mwaka 2002. Mkuu mpya wa majeshi
ya Rwanda alikuwa kamanda wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa
Mataifa UNAMID katika jimbo la Darfur nchini Sudan tangu mwaka 2009.
Mabadiliko hayo pia yamepelekea kubuniwa wadhifa mpya wa Mkaguzi Mkuu wa
jeshi uliopewa Brigedia Jenerali Jack Nziza baada ya kupandishwa cheo
na kuwa Meja Jenerali. Nziza amekuwa akihudumu kama mkurugenzi mkuu
katika wizara ya ulinzi. Pia mkuu wa zamani wa idara ya upelelezi wa nje
kanali Dany Munyuza ameteuliwa kuwa naibu kamishna mkuu wa polisi ya
Rwanda. Rais Kagame amesema mabadiliko hayo yanalenga kuimarisha huduma
kwa wananchi na vilevile kuinua hali ya usalama nchini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment