Rais Muhammad Mursi wa Misri na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Hesham
Qandil wamelaani mauaji ya Waislamu wanne wa Kishia katika eneo la Giza
yaliyofanywa hapo jana. Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Rais imelaani
mauaji hayo na kueleza kuwa, serikali haitomvumilia mtu yeyote
anayehatarisha usalama wa taifa na mshikamano wa wananchi wa Misri. Kwa
upande wake Hisham Qandil amesema kwamba tukio hilo la kinyama ni
kinyume na mafundisho ya diniya Kiislamu.
Hapo jana genge la watu
waliongozwa na viongozi wa kisalafi katika kijiji cha Zawyat Abu
Musalama, walishambulia eneo lenye wakaazi wa Kiislamu wa Kishia na
kuwaua watu wanne akiwemo shakhia mkubwa wa madhehebu hiyo.
Mahakama ya Misri imetoa waranti wa kukamatwa watu 15 waliohusika na
mauaji hayo huku uchunguzi ukiendelea. Haya yanajiri huku baadhi ya
makundi ya Misri yakimlaumu Rais Mursi kuwa, huenda matamshi yake ya
ubaguzi wa kidini aliyoyatoa hivi karibuni ndiyo yamesababisha kuuawa
Mashia hao katika eneo la Giza.
No comments:
Post a Comment