Mwana wa Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesema kwamba, hana
mpango wa kumrithi baba yake, na hivyo kukanusha tuhuma ambazo amekuwa
akielekezewa na wapinzani kwa wiki kadhaa sasa kwamba anajitayarisha
kuchukua madaraka ya nchi hiyo.
Muhoozi Kainerugaba ambaye pia ni kamanda wa vikosi maalumu amesema
kuwa, Uganda sio nchi ya kifalme ambapo uongozi hurithiwa na mtoto
kutoka kwa baba yake.
Kijana huyo mwenye miaka 39 amesema, Waganda ndio
wanaoamua Uganda iongozwe na nani, na kwamba sio mtu mmoja kama baadhi
wanavyoamini.
Mwezi uliopita polisi ya Uganda ilifunga kwa siku 10 magazeti mawili
binafsi pamoja na vituo viwili vya redio nchini humo baada ya kuripoti
mjadala wa baadhi ya majenerali wa jeshi waliodai kwamba Rais Museveni
anamtayarisha mwanaye huyo kuchukua uongozi wa nchi baada yake.
No comments:
Post a Comment