Jeshi la Lebanon limetangaza kuwa, litaendelea na oparesheni zake
kwa ajili ya kuhitimisha uasi ulioanzishwa na sheikh wa kisalafi Ahmad
al Assir na wafuasi wake waliofurutu ada, na kusababisha watu kadhaa
kuuawa. Katika taarifa yake jeshi la Lebanon limetangaza leo kuwa,
sheikh Ahmad Al Assir ndiye msababishaji mkuu wa machafuko na mapigano
huko Sweida na kumtaka yeye na wafuasi wake kueka silaha chini na kuacha
kukabiliana na jeshi.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mapigano makali bado
yanaendelea kati ya vikosi vya jeshi na wanamgambo wanaofungamana na
Ahmad al Assir sheikh mfitini wa kisalafi kwenye mji wa Sweida kusini
mwa Lebanon. Katika mapigano hayo watu wasiopungua 52 wameuawa wakiwemo
wanajeshi wa serikali.
Mapigano hayo yalianza hapo jana katika mji huo baada ya wafusi wa
sheikh huyo wa kisalafi waliofurutu ada kushambulia wanajeshi na kuwaua
watu 10 wakiwemo askari wawili. Rais Michael Suleiman wa Lebanon
amelitaka jeshi kukabiliana vilivyo na Sheikh al Assir na wafuasi wake
ili kurejesha amani na utulivu kwenye mji wa Sweida.
No comments:
Post a Comment