Uhusiano kati ya Russia na Marekani umezidi kuvurugika baada ya Moscow
kushindwa kumkamata afisa wa zamani wa CIA aliyeanika hadharani siri za
Washington wiki mbili zilizopita. Edward Snowden, hivi majuzi alifichua
kwamba Marekani imekuwa ikidukua mitandao ya intaneti kama vile Google,
Facecook, Youtube na Yahoo na kukusanya taarifa za siri za watu kote
duniani; jambo ambalo ni kinyume na sheria za kimataifa. Snowden pia
alifichua kwamba mashirika ya kijasusi ya Marekani ya CIA na NSA
yamekuwa yakinasa mazungumzo ya simu ya watu kote duniani.
Ufichuzi huo
uliamsha hasira za watu hususan huko Marekani ambako katiba ya nchi
imesisitiza kuheshimiwa faragha ya mtu. Snowden alikimbilia Hongkong
baada ya ufichuzi huo na hapo jana aliondoka na kuelekea Russia akiwa
njiani kwenda Ecuador. Washington ilikuwa imeiomba Moscow kumkamata
afisa huyo wa zamani wa CIA na kumrudisha nyumbani lakini hilo
halikufanyika. Kwa sasa Snowden ameelekea Ecuador anakotarajiwa kupata
hifadhi ya kisiasa. Wachambuzi wa mambo wanasema kwa kuzingatia jinsi
mgogoro wa Syria ulivyozigawa Marekani na Russia, kadhia ya Snowden
inatarajiwa kupanua zaidi ufa wa kidiplomasia ulioko kati ya nchi mbili
hizo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment