Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesema kuwa, serikali yake iko tayari
kutumia nguvu kurudisha amani na utulivu kaskazini mashariki mwa nchi
hiyo. Rais Kenyatta amewataka viongozi wa kikabila katika maeneo ya
Wajir, Mandera na Garissa kuyashawishi makundi yenye silaha kusalimisha
silaha hizo kwa serikali mara moja la sivyo ataliamuru jeshi na vyombo
vingine vya usalama kutumia nguvu. Kiongozi huyo ametoa onyo hilo katika
hali ambayo, maeneo hayo ya kaskazini mashariki mwa nchi yamekuwa
yakishuhudia mauaji ya kutisha dhidi ya raia na maafisa wa usalama.
Maeneo hayo yanahesabiwa kuwa hatari mno kwani yako karibu na mpaka wa
Somalia. Huku hayo yakijiri, Shirika la kimataifa la kufuatilia migogoro
ICG limetoa orodha ya nchi zinazofanya vyema na zile zinazoburuza mkia
katika masuala ya amani, uthabiti na demokrasia. Somalia imeorodheshwa
ya kwanza kama nchi hatari zaidi kiusalama duniani. Kenya licha ya
kuendesha uchaguzi wa amani mwezi Machi mwaka huu, imetajwa kuwa
miongoni mwa nchi 20 ambazo zimeshindwa kulinda demokrasia na haki za
binadamu. Uganda inashikilia nafasi ya 22. Tanzania imewekwa katika
nafasi ya 65 na kutajwa kuwa salama zaidi kushinda China na Utawala
haramu wa Israel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment