Rais Dilma Rousseff wa Brazil ameelezea uamuzi wa serikali ya
nchi hiyo wa kuitisha kura ya maoni juu ya marekebisho ya kisiasa nchini
humo.
Rais Rousseff amesema kuwa, serikali ya Brazil imeamua kuitisha kura
hiyo ya maoni kwa shabaha ya kukomesha maandamano dhidi ya serikali na
machafuko ya kijamii yaliyoikumba nchi hiyo.
Mara baada ya kufanya mazungumzo na magavana, mawaziri na mameya wa
miji yote nchini humo, Rais Rousseff ameongeza kuwa, suala la kufanyika
marekebisho ya kisiasa limekuwa likipewa kipaumbele na serikali na
kusisitiza kuwa, hivi karibuni watachaguliwa wajumbe wa jopo
litakalokuwa na jukumu la kutayarisha mchakato wa mabadiliko ya kisiasa
nchini humo.
Wananchi wa Brazil wamekuwa wakiandamana wakipinga gharama kubwa za
kuandaa fainali za kombe la dunia mwaka 2014 nchini humo, wa kunataka
kwanza iboreshwe hali ya maisha na huduma za umma kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment