Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Wednesday, June 26, 2013

37 wafa kwa kufukiwa na mgodi CAR

Watu 37 wameripotiwa kufariki dunia katika Jamhuri ya Afrika ya Kati baada ya kufunikwa na mgodi wa madini. Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati imetangaza kuwa, tukio hilo la kuporomoka mgodi wa madini ya dhahabu limetokea kilomita 440 mashariki mwa mji mkuu wa nchi hiyo Bangui na kwamba, kwa akali watu 37 wameripotiwa kupoteza maisha yao huku idadi nyingine kubwa ya watu wakijeruhiwa. Taarifa za awali zinasema kuwa, mvua kubwa iliyofuatiwa na mafuriko ndiyo iliyosababisha kuporomoka kwa mgodi huo wa madini.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, kazi ya uokozi inaendelea kwa ajili ya kujaribu kuokoa maisha ya wafanyakazi wa mgodi huo wa madini ambao wamefukiwa na kifusi cha udongo.

No comments: