Mshauri wa Waziri Mkuu wa serikali iliyochaguliwa na wananchi wa
Palestina, amesema kuwa, Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina
(Hamas), bado ina mahusiano mazuri na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya nchini Lebanon. Basim
Naim ameyasema hayo leo katika mahojiano yake na Shirika la Habari la
Lebanon la an-Nashrah na kuongeza kuwa, Harakati ya Hamas itaendelea
kushirikiana kwa karibu na kila yule anayeisaidia harakati hiyo kwa
namna moja ama nyingine hususan Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na
Hizbullah. Basim amesisitiza kuwa, harakati ya Hamas haitatoa mwanya kwa
adui kuuzorotesha muqawama kwa kuzusha tofauti zinazoweza kuharibu
uhusiano wake na Tehran na vilevile Harakati ya Hizbullah. Wakati huo
huo, kiongozi wa ngazi za juu wa Harakati hiyo ya Hamas Mahmud Az Zahar
amezungumzia kadhia ya Syria na kusisitiza kuwa, kubakia Syria yenye
nguvu na kuwepo uhusiano mwema na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na
Hizbullah ni suala lenye muhimu mkubwa katika eneo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment