Wimbi jipya la mapigano mapya kati ya makabila hasimu
yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 11 huko Darfur, magharibi mwa
Sudan. Watu walioshuhudia wamesema kuwa mapigano makali yaliibuka juzi
katika eneo la Edd al Fursan umbali w akilomita 100 kusini magharibi
mwa Nyala makao makuu ya jimbo la Darfur Kusini.
Watu hao waliuliwa baada ya watu wa kabila la Beni Halba
kuvishambulia vijiji vya wenzao wa kabila Gimir katika eneo hilo.
Kiongozi wa kabila la Gimir ameeleza kuwa watu wa kabila la Beni Halba
walivamia na kushambulia vijiji vyao wakiwa na magari, pikipiki ,
farasi, ngamia na silaha nzito na kwamba wenzao watano wameuawa katika
mapigano.
Naye mkuu wa kabila la Beni Halba amesema kuwa, watu sita wa kabila
lao wameuawa kwenye mapigano hayo. Amesema wanapigana ili kulinda ardhi
yao.
No comments:
Post a Comment