Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kitaanza operesheni
zake nchini Mali ifikapo Julai Mosi mwaka huu baada ya Baraza la
Usalama la umoja huo kutoa kibali hapo jana kwa kikosi hicho.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lenye nchi wanachama 15 mwezi
Aprili liliafiki kutumwa kikosi hicho cha askari jeshi 12,600
kinachojulikana kwa jina la Minusma.
Wanajeshi wa Ufaransa watakisaidia kikosi hicho cha Umoja wa Mataifa
katika kupambana na waasi wa kaskazini mwa Mali iwapo itahitajika.
Ufaransa ikisaidiwa na wanajeshi elfu mbili wa Chad ilianzisha uvamizi
wa kijeshi huko Mali kwa kile ilichokitaja kuwa mapambano ya
kuwatokomeza waasi wa kaskazini mwa Mali.
No comments:
Post a Comment