Mzee Nelson Mandela rais wa kwanza wa Afrika Kusini baada ya utawala wa
ubaguzi wa rangi amelazwa tena hospitali akisumbuliwa na maradhi ya
mapafu. Taarifa iliyotolewa na ofisi ya rais imeeleza kuwa, hali yake ni
mbaya lakini imedhibitiwa na kwamba anaweza kupumua mwenyewe, suala
linaloleta matumaini. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mandela mwenye umri
wa miaka 94 ambaye mwezi Aprili alilazwa hospitalini kutokana na
matatizo ya kupumua, amekuwa akisumbuliwa tena na ugonjwa huo katika
siku kadhaa zilizopita. Taarifa hiyo imeongeza kuwa, leo asubuhi Mzee
Mandela alipelekwa hospitali mjini Pretoria baada ya kuzidiwa na kwamba
madaktari wanafanya jitihada za kumtibu ili apate nafuu.
Rais Jacob Zuma
kupitia mtandao wa tweeter amesema kwa niaba ya wananchi wa Afrika
Kusini kwamba anamuombea mzee Madiba apate afueni haraka na kuvitaka
vyombo vya habari na umma kwa ujumla kuheshimu faragha ya rais huyo wa
zamani wa Afrika Kusini na familia yake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment