Waziri Mkuu mpya wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina aliyejiuzulu, Rami
Hamdallah, amepinga ombi la kumtaka abadili msimamo wake wa kujiuzulu
wadhifa huo. Hii ni katika hali ambayo mazungumzo ya leo kati ya waziri
mkuu huyo aliyetangaza kung’atuka madarakani baada ya kuhudumu katika
nafasi hiyo kwa muda wa chini ya wiki mbili, na Tayeb Abdul Rahim
Mshauri Mkuu wa Mahmoud Abbas Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina na
Majid Faraj Mkuu wa Idara ya Kiintelijensia ya Mamlaka hiyo,
yamemalizika bila kufikiwa natija yoyote.
Duru za habari zinaarifu kuwa,
katika mazungumzo hayo Tayeb Abdul Rahim na Majid Faraj walikuwa
wakimtaka Hamdallah abadili msimamo wake wa kujiuzulu na kumuomba
aendelee katika nafasi hiyo. Tofauti kati ya waziri mkuu huyo na manaibu
wake, zinatajwa kuwa chanzo cha kujiuzulu kwake. Rami Hamdallah
aliteuliwa kuchukua nafasi ya mtangulizi wake, Salam Fayadh aliyejiuzulu
mwezi Aprili, tarehe sita mwezi huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment