Bunge la Libya limemchagua Nouri Abusahmain kuwa spika mpya kufuatia
kujiuzulu mtangulizi wake, Mohammed Magarief. Abusahmain ambaye anatoka
katika kabila la wachache alijipatia kura 96 huku mpinzani wake wa
karibu, Al-Sharif al-Wafi akijipatia kura 80. Magarief alijiuzulu
kufuatia kupitishwa sheria inayopinga watu waliohudumu katika serikali
ya Muammar Gaddafi kushikilia nyadhifa zozote za umma. Ingawa Magarief
aliwahi kuhudumu katika serikali ya Gaddafi, alikuwa na mchango mkubwa
katika mapinduzi yaliyopelekea kupinduliwa dikteta huyo mwaka 2011.
Sheria hiyo mpya inasisitiza kuwa, kila aliyehudumu chini ya Gaddafi
hafai kushikilia wadhifa wowote hata kama alimpinga dikteta huyo wakati
wa harakati za mapinduzi. Spika mya ataongoza kamati itakayotayarisha
rasimu ya katiba mpya ambayo baada ya kukamilika, itapigiwa kura na
wananchi. Katiba mpya itatoa fursa ya kufanyika uchaguzi wa rais na
kuirudisha Libya katika hali ya kawaida kisiasa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment