Siku moja baada ya kutwaa rasmi madaraka ya nchi, Amir mpya wa Qatar,
Sheikh Tamim bin Hamad al-Thani anatarajiwa kumteua Waziri Mkuu mpya
atakayekuwa na dhima ya kuunda serikali mpya ya nchi hiyo. Duru
zimefichua kwamba, Amir mpya huenda akamteua Waziri wa sasa wa Mambo ya
Ndani, Sheikh Abdullah bin Nasser bin Khalifa al-Thani kuwa Waziri Mkuu
mpya.
Waziri Mkuu wa sasa, Sheikh Hamad bin Jassim al-Thani amesema yuko
tayari kuachia ngazi ili vijana waingie madarakani na kulisukuma mbele
gurudumu la taifa. Hapo jana, Sheikh Hamad bin Khalifa al-Thani
alitangaza rasmi kustaafu na kukabidhi rasmi madaraka ya nchi kwa
mwanaye. Mfumo wa utawala nchini Qatar ni ule wa kifalme ambapo familia
ya Aal Thani ndiyo yenye kutawala nchi hiyo. Nchi hiyo ndogo ya Ghuba ya
Uajemi ni muitifaki wa karibu wa Marekani na katika miaka ya hivi
karibuni imekuwa ikiunga mkono magaidi wanaopigana na serikali nchini
Syria sambamba na kuwapa misaada ya fedha na silaha magaidi hao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment