Mjumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu
katika mgogoro wa Syria, al-Akhdhar Brahimi amesema wale wanaoendelea
kusambaza silaha nchini Syria ndio wachochezi wakubwa wa mgogoro uliko
nchini humo. Mwanadiplomasia huyo amesema kuwa, mgogoro wa Syria
utakwisha punde nchi mbalimbali zitakapokoma kusambaza silaha kwa pande
zinazohasimiana.
Brahim aidha ameelezea hofu yake kuhusu mazungumzo
yajayo huko Geneva akisema Marekani na Russia bado hazijaonyesha irada
thabiti ya kisiasa ya kusimamia mkutano huo. Amesema huenda mkutano huo
uliopewa jina la Geneva 2 usifanyike mwezi ujao wa Julai kutokana na
kuendelea kutokota mgogoro wa Syria. Hii ni katika hali ambayo, siku
chache zilizopita, serikali ya Damascus ilitangaza kuwa iko tayari
kushiriki mkutano huo na kuutaka upande wa pili pia kushiriki bila
masharti yoyote. Weledi wa mambo wanasema hatua ya Marekani na baadhi ya
nchi za Kiarabu ya kuendelea kuwapa silaha magaidi ndiyo sababu
inayopelekea wao kuvimba kichwa na kukataa kushiriki kwenye mazungumzo
yoyote ya amani na serikali ya Syria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment