Mkuu wa harakati ya Uadilifu na Usawa ya nchini Sudan ametangaza
utayarifu wake wa kufanya mazungumzo na serikali ya Sudan kwa lengo la
kufikiwa makubaliano ya amani ya mjini Doha sambamba na kuimarisha
usalama katika eneo hilo. Mkuu wa Harakati hiyo Muhammad Bashar amesema
kuwa, wamechukua hatua hiyo kwa ajili ya kuwadhaminia amani wakazi wa
jimbo hilo la Darfur na kwamba, pamoja na kwamba, makubaliano ya mjini
Doha hayawezi kukidhi matakwa muhimu ya wakazi wa jimbo hilo, lakini
usalama na amani ni msingi mkuu wa mahitaji ya wakazi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment